pic_-26-3e3e7

Ndayishimiye Amshutumu Rwanda Tena Katika Mkutano wa Kampala

Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye, siku ya Jumatano aliendelea kulishutumu Rwanda kwa kuchochea hali ya ukosefu wa usalama katika ukanda wa Maziwa Makuu.

Ametoa kauli hiyo kali jijini Kampala, Uganda, alipokuwa akihutubia Mkutano wa 12 wa Ngazi ya Juu wa Mfumo wa Uangalizi wa Kanda kuhusu Amani, Usalama na Ushirikiano kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), unaoendelea huko Entebbe.

Katika hotuba yake, alilishukuru jumuiya ya kimataifa kwa kulaani mashambulizi ya waasi wa M23 na madai ya ushiriki wa majeshi ya Rwanda katika vita vya Kivu Kaskazini na Kusini.

Alisema:

“Napenda kushukuru majibu ya haraka kutoka kwa mashirika mbalimbali ya kimataifa, hasa Azimio la 2773 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ambalo lililaani vikali mashambulizi yanayoongozwa na M23 katika Kivu ya Kaskazini na Kusini kwa msaada wa majeshi ya Rwanda, pamoja na kuanguka kwa miji ya Goma na Bukavu.”

Aliongeza kuwa anapongeza pia mikutano mbalimbali ya bara la Afrika ambayo ililaani mauaji anayoamini yamefanywa na M23 na RDF (Jeshi la Ulinzi la Rwanda).

Ndayishimiye aliwaomba washiriki wa mkutano huo kutafuta suluhisho la haraka kwa mgogoro wa mashariki mwa DRC, akisema kuwa ikiwa hatua hazitachukuliwa, vita hivyo vinaweza kusambaa zaidi.

“Kwa sasa tunapozungumza, vita vya mashariki mwa DRC vimefikia kilele chake. Bila hatua za haraka, kuna hatari ya vita hivyo kusambaa katika majimbo mengine ya DRC, na hata kuathiri nchi zingine za ukanda wa Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.”

Alisema kuwa vikundi vya waasi wa kigeni vinavyosaidiwa na mataifa kama Rwanda vinapaswa kudhibitiwa.

“Vikundi hivi vya waasi wa kigeni vinavyofanya kazi mashariki mwa DRC vinasaidiwa na nchi kama Rwanda, na vinajaribu kunufaika na hali ya sasa. Nimepata fursa ya kuhamasisha jamii ya kimataifa na kanda kuhusu maeneo yanayotekwa kila siku yanayohatarisha utulivu wa kanda.”

Neva (Ndayishimiye) alisema kuwa athari za vita vya DRC si ongezeko la wakimbizi tu, bali pia ni kuongezeka kwa uhalifu na usafirishaji haramu wa silaha, hali ambayo inaweza kuingiza mataifa mengine kwenye mzozo.

Matamshi haya ya kumshutumu Rwanda yanakuja baada ya Rais huyo wa Burundi kusema hivi karibuni kuwa yuko tayari kuingia vitani na nchi hiyo jirani.

Sangiza iyi nkuru

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *