franck-ribery-and-cristiano-ronaldo

Frank Ribéry Amcheka Cristiano Ronaldo Kuhusu Ballon d’Or

Mfaransa Frank Ribéry amemdharau Cristiano Ronaldo baada ya Mreno huyo kusema kuwa, kwa maoni yake, Ballon d’Or inapaswa kupewa mchezaji aliyeshinda Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League).

Kwa sasa, mijadala inaendelea kuhusu nani anastahili kushinda Ballon d’Or ya mwaka huu, baada ya kumalizika kwa msimu wa mpira wa miguu wa 2024/25.

Mfaransa Ousmane Dembélé aliyeshinda makombe mbalimbali na Paris Saint-Germain ikiwemo UEFA Champions League, na Mhispania Lamine Yamal aliyekuwa na mwaka wa kipekee, ni miongoni mwa wanaotajwa kuwa kwenye mbio za tuzo hiyo inayotolewa na jarida la France Football.

Mjadala umezidi kushika kasi baada ya Yamal na timu ya taifa ya Uhispania kuwaondoa Wafaransa wa Dembélé katika UEFA Nations League.

Cristiano Ronaldo, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Jumamosi kabla ya fainali ya Nations League kati ya Ureno na Uhispania, aliulizwa nani anastahili kushinda Ballon d’Or ya mwaka huu.

Mshambuliaji wa Al Nassr alijibu kuwa hataki kutaja jina, lakini kwa mtazamo wake, tuzo hiyo inapaswa kwenda kwa mshindi wa UEFA Champions League.

Akasema: “Kwangu mimi, Ballon d’Or inapaswa kila mara kwenda kwa mchezaji aliyeshinda Ligi ya Mabingwa. Nafikiri tuzo hii imepoteza thamani yake.”

Kauli hizi zimezua sintofahamu ikizingatiwa kuwa Ronaldo aliwahi kushinda Ballon d’Or mwaka 2013 licha ya kwamba Real Madrid haikushinda UEFA Champions League. Mwaka huo, Bayern Munich ndio walishinda, na wengi waliamini kuwa Franck Ribéry ndiye aliyestahili kushinda tuzo hiyo.

Ribéry alionekana kuthibitisha hilo kwa kumkejeli Ronaldo kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Aliandika: “Unahitaji kushinda UEFA Champions League ili ushinde Ballon d’Or?”
Ujumbe huo uliambatana na emojis za kucheka.

Tuzo ya Ballon d’Or ya mwaka huu itatolewa tarehe 22 Septemba.

Sangiza iyi nkuru

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *