Kila tarehe 30 Juni, dunia huadhimisha Siku ya Kimataifa ya Asteroidi. Hii si siku ya sherehe, bali ya kutafakari kwamba dunia tunayoiishi si mahali salama kabisa.
Anga letu limejaa gesi mbalimbali na mawe madogo ya angani (asteroidi) yanayozunguka kwenye nafasi, ambayo yanaweza kugonga Dunia wakati wowote.
Hii si hadithi ya kutisha bali ni ukweli. Tarehe hiyo huadhimishwa kwa kumbukumbu ya tukio la Tunguska, ambapo mwaka 1908 jiwe la angani lililipuka juu ya msitu huko Siberia na kuharibu eneo la zaidi ya km² 2,000.
Hili ndilo tukio kubwa la asteroidi kuwahi kurekodiwa katika historia ya karibuni.
Tangu wakati huo, wanasayansi, mashirika ya anga na Umoja wa Mataifa walianza kuchukua suala la asteroidi kwa uzito mkubwa.
🪨 Asteroidi ni nini?
Ni miamba midogo inayopatikana kati ya sayari ya Mars na Jupiter. Wanaweza kuwa na kipenyo cha sentimita chache hadi kilomita kadhaa.
Inapogonga Dunia, husababisha madhara makubwa kama mlipuko, tsunami, moto, au mabadiliko ya hali ya hewa.
Athari zake ni sawa na za silaha za nyuklia, ila kwa muda mrefu zaidi.
☄️ Matukio ya kihistoria:
Chicxulub (Mexico, miaka milioni 66 iliyopita): Asteroidi iliyoangamiza dinosaur.
Tunguska (Siberia, 1908): Msitu wa km² 2,000 uliharibiwa.
Chelyabinsk (Urusi, 2013): Watu 1,500 walijeruhiwa, madirisha 7,000 yakavunjika.
Hoba (Namibia): Jiwe la tani 60 lilidondoka ardhini bila madhara makubwa, lakini lilionyesha hatari iliyopo.
🛡️ Je Dunia inaweza kujilinda?
Ndiyo. Kuna njia mbalimbali:
Kinetic Impactor – (DART mission 2022)
Miale ya jua au laser – kubadilisha mwelekeo
Gravity Tractor – satelaiti inayovuta asteroidi mbali
Silaha za nyuklia – chaguo hatari sana
Tarehe 30 Juni si kwa ajili ya huzuni bali ni saa ya kujifunza, kujiandaa, na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa kulinda sayari yetu.




