photos__7-77-56826-3

Rwanda Yapandisha Tena Bei ya Mafuta Kuanzia Julai 2

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Umma ya Rwanda (RURA) imetangaza kuwa kuanzia Jumatano, tarehe 2 Julai 2025, saa 12:00 asubuhi, bei za juu za bidhaa za mafuta ya petroli zitapanda rasmi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyosainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa RURA, Bw. RUGIGANA Evariste, bei ya petroli haipaswi kuzidi RWF 1,803 kwa lita, na bei ya dizeli haipaswi kuzidi RWF 1,757 kwa lita. Bei hizi zinajumuisha Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT).

RURA imesema kupanda kwa bei hii kunatokana na mabadiliko ya bei katika soko la dunia, lakini Serikali ya Rwanda inaendelea kutoa ruzuku kwa bidhaa za mafuta ili kupunguza mzigo kwa wananchi, hasa kwenye sekta za usafirishaji na uzalishaji wa kiuchumi.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa serikali bado imejitolea kulinda hali ya maisha ya wananchi kwa kupunguza athari za ongezeko la mafuta, ili kuepusha madhara kwa uchumi wa taifa.

Ongezeko hili linakuja miezi miwili tu baada ya lile la awali, huku mataifa mengi duniani yakiendelea kukumbwa na matatizo ya vita, misukosuko ya kiuchumi, na mabadiliko ya thamani ya dola ya Marekani.

Sangiza iyi nkuru

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *