Wachezaji watatu wa timu ya wanawake ya Arsenal — Katie McCabe, Caitlin Foord na Laia Codina — waliwasili nchini Rwanda siku ya Jumatatu, tarehe 8 Julai 2025, kwa ziara ya siku nne itakayohitimika tarehe 11 Julai 2025.
Asubuhi ya Jumanne, wachezaji hao waliwasili Rwanda kwa lengo la kuitangaza nchi hiyo kama kivutio cha utalii kupitia kampeni ya Visit Rwanda.
Wakiwa nchini humo, wachezaji hao watatembelea Hifadhi ya Taifa ya Akagera na kujifunza kuhusu utamaduni, historia na maendeleo ya Rwanda.
Ushirikiano kati ya Arsenal na Rwanda ulianza Mei 2018, ambapo timu ya wanaume ya wakubwa, wanawake na ile ya chini ya miaka 23 huvaa nembo ya Visit Rwanda kwenye bega la kushoto la jezi zao.
Uhusiano huu unaendelea kusaidia Rwanda kujitangaza kimataifa kupitia ushirikiano na vilabu mashuhuri vya soka duniani.





