d5de791f778e495393a55380fd996b10_md_1753135507

A$AP Rocky Aonekana Akiwa Kwenye Kiti cha Magurudumu: Wasiwasi Wazuka Kuhusu Afya Yake

Msanii mashuhuri wa muziki wa Hip Hop kutoka Marekani, A$AP Rocky, ambaye pia ni mume wa Rihanna, ameonekana hadharani akiwa kwenye kiti cha magurudumu, amefunikwa kwa kitambaa na akisindikizwa na walinzi wake waliomsaidia kuingia kwenye gari lake la kifahari aina ya Hummer huko West Hollywood.

Kwa mujibu wa TMZ, tukio hili limetokea baada ya Rocky kurejea Marekani akitoka katika maonyesho makubwa ya burudani, yakiwemo yaliyofanyika kwenye wiki ya mitindo mjini Paris.

Hakuna taarifa kamili kuhusu ugonjwa anaoweza kuwa nao, lakini picha na video zinazozunguka kwenye mitandao ya kijamii zimezua wasiwasi mkubwa miongoni mwa mashabiki, hasa kutokana na muonekano wake wa kuchoka.

Wataalamu wa burudani wanasema huenda anapumzika baada ya kipindi cha safari nyingi na maonesho makubwa yaliyomchosha.

Hata hivyo, wawakilishi wa Rocky na familia ya Rihanna hawajatoa taarifa yoyote rasmi kuhusu hali yake ya afya.

Sangiza iyi nkuru

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *