IRAN-MILITARY

Iran Yaomboleza: Mazishi ya Kitaifa ya Watu 60 Waliouawa Kwenye Vita vya Siku 12 na Israel

Jumamosi, tarehe 28 Juni 2025, Iran iliandaa hafla ya mazishi kwa watu wapatao 60, wakiwemo makamanda wa kijeshi wa ngazi ya juu na wanasayansi wa nyuklia, waliouawa kwenye vita vya siku 12 dhidi ya Israel.

Majeneza yaliyofunikwa kwa bendera ya Iran na picha za marehemu yaliwekwa karibu na Uwanja wa Enghelab jijini Tehran, yakiwa yamezungukwa na umati mkubwa wa waombolezaji.

Mapigano hayo yalimalizika mapema wiki hii kwa makubaliano ya kusitisha vita, baada ya Marekani kushambulia moja kwa moja vituo vya utafiti wa nyuklia nchini Iran.

Umati wa watu waliovaa mavazi meusi waliimba nyimbo za huzuni, wakipeperusha bendera za Iran na kubeba picha za waliouawa vitani.

Kabla ya hafla hiyo, vyombo vya habari vya serikali vilihamasisha wananchi kuhudhuria kwa wingi, huku mabasi na treni zikitolewa bure. Ofisi za serikali zilifungwa kwa siku nzima.

Miongoni mwa waliozikwa ni Mohammad Bagheri, jenerali wa ngazi ya juu na Mkuu wa Majeshi ya Iran.

Bagheri alizikwa pamoja na mkewe na binti yake waliouawa katika shambulio la Israel. Jumla ya watu 627 wanaripotiwa kuuawa nchini Iran, kulingana na viongozi wa serikali.

Viongozi wa Israel wamesema kuwa watu 28 waliuawa nchini Israel kutokana na mashambulizi ya kombora kutoka Iran, kulingana na ripoti ya BBC.

Pia walizikwa Hossein Salami, aliyekuwa Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, na Mohammad Mehdi Tehranchi, mwanasayansi wa nyuklia na mkuu wa Chuo Kikuu cha Azad mjini Tehran.

Sangiza iyi nkuru

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *