20250621_214246

Jenerali Muhoozi Awaonya Wazalendo Baada ya Ziara Kinshasa, Amsifu Kagame

Kamanda Mkuu wa Majeshi ya Uganda, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, ameikosoa vikali makundi ya Wazalendo yanayoungwa mkono na serikali ya DRC katika vita dhidi ya M23, akiyataja kuwa makundi yenye nia mbaya.

Muhoozi alitoa matamshi haya baada ya kurejea kutoka Kinshasa, alikokutana na Rais Félix Antoine Tshisekedi.

Ziara hiyo ilisababisha makubaliano mapya ya ushirikiano wa kijeshi kati ya UPDF na FARDC, yanayoruhusu Uganda kuwashambulia waasi walioko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Kupitia ukurasa wake rasmi wa X (zamani Twitter), Muhoozi aliwatangaza Wazalendo kama hatari kwa usalama, na akasema watashambuliwa popote walipo iwapo hawatajisalimisha.

“Wazalendo ni makundi ya kishetani kabisa! Niaminini, majeshi ya pamoja ya UPDF na FARDC yatawashambulia kila walipo, isipokuwa wakiamua kujisalimisha kwa hekima.”

Pia aliwatuhumu kwa kuwaua raia, hasa wanaoishi karibu na mpaka wa Uganda na DRC.

“Hatutasubiri. Mkimuua raia wetu, mtalipa kwa hilo.”

Sifa Kwa Kagame

Katika ujumbe mwingine, Muhoozi alimsifu tena Rais wa Rwanda, Paul Kagame, akisema bado ni shujaa wake, akikanusha madai kuwa amemsaliti Rwanda kwa kukaribia DRC.

Akiambatanisha picha ya Kagame, aliandika:

“Bado ni shujaa wangu. Mapenzi yaendelee!”

Na kuongeza kwa ukali:

“Yeyote anayeamini kuwa nimewahi kutofautiana na ‘mjomba wangu’ Paul Kagame, na aende moja kwa moja kuzimu.”

Sangiza iyi nkuru

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *