20250418_200026

Joseph Kabila aliyekuwa amekimbia kutoka DRC, alipitia Kigali kuelekea Goma

Joseph Kabila Kabange, rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), amewasili katika mji wa Goma baada ya kurejea kutoka uhamishoni.

Kabila, aliyelitawala taifa hilo kwa miaka 18 kabla ya kumkabidhi madaraka Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo, alikuwa ameishi uhamishoni Harare, Zimbabwe kwa mwaka mmoja.

Mnamo Jumanne, tarehe 8 Aprili, alitangaza kuwa anarejea nchini DRC.

Wakati huo alisema amefanya uamuzi huo kwa sababu nchi ilikuwa katika hali mbaya ya usalama “na katika sekta nyingine zote za maisha ya taifa,” kwa lengo la kusaidia kutafuta suluhisho.

Kabila alisema kuwa akirejea nchini, angeanzia mashariki mwa DRC, ambako mapigano yanaendelea kati ya jeshi la serikali na waasi wa M23.

Ripoti zinasema alifika Goma siku ya Ijumaa tarehe 18 Aprili, baada ya kupita Kigali.

Mji wa Goma, ambako Kabila amewasili, unadhibitiwa na waasi wa M23 tangu mwisho wa Januari mwaka huu.

Hii ilitokea baada ya jeshi la serikali kufurushwa kutoka eneo hilo.

Kuna taarifa kwamba Kabila anaweza kuungana na muungano wa Alliance Fleuve Congo (AFC), ambao unajumuisha M23. AFC inaongozwa na Corneille Nangaa, aliyekuwa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi wakati wa utawala wa Kabila.

Joseph Kabila amerudi DRC katika wakati ambapo uhusiano wake na Rais Tshisekedi ni wa mivutano.

Tshisekedi amemshutumu mara kwa mara kuwa ndiye mdhamini mkuu wa kundi la M23.

Inatarajiwa kuwa Rais wa zamani atalihutubia taifa la Congo siku ya Jumamosi, akizungumza kutoka mjini Goma, ambao ni mji mkuu wa Mkoa wa Kivu Kaskazini.

Sangiza iyi nkuru

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *