Captured’écran2025-05-23à20.41.09_copy_888x666

Joseph Kabila Asema Hadharani: “Ninaelekea Goma Karibuni

Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Joseph Kabila Kabange, amekanusha taarifa zilizodai kwamba tayari yuko katika jiji la Goma, akibainisha kuwa atakielekea siku chache zijazo.

Kabila alitoa kauli hiyo katika hotuba kwa wananchi wa Kongo aliyotoa usiku uliopita.

Hotuba hiyo ilitolewa saa chache baada ya Seneti ya DRC kumvua kinga ya ubunge wa maisha, hivyo kuruhusu kufunguliwa mashtaka dhidi yake mahakamani.

Inatarajiwa kuwa Mahakama Kuu ya Kijeshi itaanza kesi dhidi yake hivi karibuni, ikimhusisha na mashtaka ya kushiriki njama ya kupindua serikali pamoja na uhaini.

Mashtaka hayo yalijitokeza baada ya ripoti kwamba Kabila alionekana Goma, jiji linalodhibitiwa na waasi wa M23, ambao serikali ya Kinshasa imekuwa ikimtuhumu kuwaunga mkono.

Katika hotuba yake, Kabila alikana kuwa amewahi kuwa Goma, kinyume na madai yaliyosambaa.

Alisema kuwa maamuzi ya serikali ya kumshtaki, kutaifisha mali zake zote, na kufungia chama chake cha PPRD, yalifanywa kwa haraka na bila busara, kutokana na uvumi wa kuwa ameenda eneo linalodhibitiwa na M23.

Alisema:

“Kama ukweli ndio tunautafuta, basi na upewe tena. Siku chache zilizopita, baada ya uvumi mdogo kuenea mitaani na mitandaoni kwamba niko Goma — mji nitakaoelekea hivi karibuni — serikali ya Kinshasa ilifanya maamuzi ya haraka na ya kutisha. Hili linaonyesha wazi jinsi demokrasia inavyozidi kudhoofika nchini mwetu.”

Kabila pia alishutumu serikali ya DRC kwa kuwasaliti na kuwadharau wananchi wa mashariki mwa nchi, kwa kufunga huduma muhimu kama benki na usafiri.

Alisema hatua hizo ni sawa na kuwakandamiza watu wa mashariki na kuwaweka katika hatari kubwa isiyowahi kushuhudiwa.

Joseph Kabila alikuwa Rais wa DRC kati ya 2001 hadi 2019.
Hii ni mara ya kwanza kwa Kabila kuzungumza hadharani tangu aingie kwenye uhamisho wa hiari, baada ya kumkabidhi madaraka Rais Félix Antoine Tshisekedi, ingawa waligombana muda mfupi baadaye.

Sangiza iyi nkuru

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *