20250507_122722

Kagame na Macron Wakutana Paris: Ushirikiano Waimarishwa Kabla ya Mechi Kati ya PSG na Arsenal

Rais Paul Kagame alikutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, siku ya Jumatano tarehe 7 Mei.

Viongozi hao wawili walikutana katika Ikulu ya Rais wa Ufaransa, Champ Elysée.

Ofisi ya Rais wa Rwanda ilitangaza kuwa Kagame na Macron “walijadili masuala ya kimataifa na ushirikiano wenye matokeo chanya” kati ya Rwanda na Ufaransa.

Ziara ya mwisho ya Rais Kagame nchini Ufaransa ilikuwa mwezi Oktoba 2024, alipohudhuria mkutano wa Francophonie. Wakati huo pia alikutana na Macron na wakazungumzia changamoto za usalama katika mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Baada ya mazungumzo na Macron, inatarajiwa kuwa Rais Kagame atahudhuria mechi ya nusu fainali ya UEFA Champions League siku hiyo jioni, ambapo Paris Saint-Germain watakuwa wenyeji wa Arsenal — timu zote mbili zikiwa na ushirikiano na Rwanda kupitia kampeni ya Visit Rwanda.

Sangiza iyi nkuru

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *