Mwanamke wa miaka 27 kutoka Australia aitwaye Annie Knight, anayefahamika sana kupitia jukwaa la OnlyFans, amelazwa hospitalini ghafla baada ya kujaribu kuweka rekodi kwa kulala na wanaume 583 ndani ya saa sita tu.
Tukio hilo lilifanyika jijini Sydney, ambapo aliandaa shughuli hiyo kwa lengo la kuonyesha “uwezo wa mwili wake” na kutengeneza video kwa ajili ya akaunti yake. Awali alilenga wanaume 200, lakini idadi hiyo ilipanda hadi kufikia 583.
Baada ya muda mfupi, Annie alianza kuonyesha dalili za kupoteza damu kwa kiwango kikubwa pamoja na madhara kwenye sehemu za siri, hali iliyomlazimu kukimbizwa hospitalini. Daktari Zac Turner, mtaalamu wa afya ya jumla, alisema kuwa tabia kama hizo zinaweza kuwa na athari kubwa kwa mwili na akili ya binadamu.
“Mwili wa binadamu haukuumbwa kustahimili shughuli kama hizo kwa muda mfupi sana. Ingawa ngono ni sehemu ya maisha yenye afya, ikizidi kiasi inaweza kusababisha madhara ya mwili na akili,” alisema daktari huyo.
Ingawa Annie alikuwa akitumia dawa za maumivu na kuzuia kutokwa na damu, kiwango cha kile alichopitia kilikuwa kikubwa mno na kilizidi uwezo wa dawa hizo.
Kupitia ujumbe aliouweka kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuruhusiwa hospitalini, Annie alitangaza kuacha kutengeneza maudhui ya ngono, ili aweke kipaumbele kwenye afya yake.
“Nimetambua kwamba afya yangu ndiyo ya kwanza. Nahitaji muda wa kujitunza na kuuweka mwili wangu sawa,” alisema.
Kwa sasa yuko na mpenzi wake Henry Brayshaw, na anasema kuwa anazingatia mahusiano yao na kuishi maisha ya kawaida.
Licha ya kuacha kazi hiyo, Annie bado ni tajiri, akidaiwa kupata angalau dola 200,000 kwa mwezi na kumiliki nyumba nne.




