98559545-0-image-a-51_1747728972635

Lamine Yamal Kurithi Jezi ya Messi – Nyota Chipukizi wa Barcelona Apewa Heshima Kubwa

Mchezaji kinda wa Uhispania, Lamine Yamal, anaripotiwa kuwa karibu kupewa nambari ya jezi ya hadhi ya Lionel Messi katika klabu ya FC Barcelona, baada ya kufikia makubaliano ya mkataba mpya wa muda mrefu.

Kwa mujibu wa tovuti ya Memorabilia1899.co, Yamal mwenye umri wa miaka 17 anatarajiwa kusaini mkataba mpya mwezi Julai, atakapofikisha miaka 18.

Mkataba huo utaambatana na kipengele cha kumruhusu kuondoka kwa euro bilioni moja (€1,000,000,000), sawa na trilioni 1.4 za faranga za Rwanda, kulingana na viwango vya sasa vya ubadilishaji wa fedha.

Yamal kwa sasa huvaa jezi nambari 19, ambayo pia Messi alivaa kabla ya kupewa nambari 10 mwaka 2008. Atachukua nafasi ya Ansu Fati, ambaye hatma yake ndani ya Barcelona haijulikani.

Yamal alianza kuchezea kikosi cha kwanza cha Barcelona akiwa na miaka 15, na tayari ameshinda mataji mawili ya La Liga, akichangia mabao 43 katika mechi 54 – ishara tosha ya kipaji chake kikubwa.

Mwaka jana, aliisaidia timu ya taifa ya Uhispania kushinda taji la Ulaya (EURO), na sasa amejumuishwa miongoni mwa wanaowania tuzo ya Ballon d’Or, licha ya kuwa bado ni mdogo.

Kupokea jezi ya Messi ni hatua kubwa kwa kijana huyu aliyelelewa kwenye La Masia, kituo maarufu cha kukuza vipaji cha FC Barcelona kinachozalisha wachezaji wa kiwango cha dunia.

Sangiza iyi nkuru

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *