Carte Walikale2

M23 Yapata Wanajeshi Wapya 8,000 Baada ya Mafunzo ya Miezi Sita

Kundi la waasi la M23 limeongeza zaidi ya wanajeshi 8,000 wapya baada ya kumaliza mafunzo ya kijeshi ya miezi sita.

Mafunzo hayo yalifanyika katika kambi ya kijeshi ya Chanzu, iliyoko katika eneo la Rutshuru.

Wanajeshi hao ni pamoja na maafisa wa zamani wa jeshi la serikali ya Congo (FARDC) waliokimbilia M23 mwezi Januari mwaka huu, baada ya kundi hilo kuwashinda katika mapigano na kuchukua mji wa Goma.

Taarifa zinaeleza kuwa mara baada ya mafunzo kumalizika, wanajeshi hao walitumwa mkoa wa Kivu Kusini, ambapo malori mengi yaliwasili mji wa Bukavu yakiwa yamewabeba kutoka Goma.

Inasemekana kwamba M23 inapanga kuiteka mji wa Uvira, ambao ni mji wa pili kwa ukubwa katika Kivu Kusini, jambo linaloeleza kwa nini wanajeshi hao wamepelekwa karibu na eneo hilo.

Mnamo Februari, wakati wa ziara yao kwenye kambi ya Rumangabo, Kamanda Mkuu wa M23, Jenerali Sultani Makenga, aliwaambia wanajeshi hao kwamba “watasafishwa hofu waliyoingiziwa na Tshisekedi,” na kwamba kazi inayowasubiri ni “kuikomboa Congo na watu wake.”

Sangiza iyi nkuru

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *