20250510_101803

M23 Yatoa Siku 7 kwa FARDC na Wazalendo Kujisalimisha Walungu

Ijumaa hii, kundi la waasi wa M23 limetoa makataa ya siku saba kwa wanajeshi wa FARDC na wapiganaji wa Wazalendo wanaojificha katika maeneo mbalimbali ya Tarafa ya Walungu, kuwataka waweke silaha chini.

Walungu, iliyoko katika Mkoa wa Kivu Kusini, imekuwa uwanja wa mapigano ya mara kwa mara tangu Februari mwaka huu kati ya M23 na wapiganaji wa Wazalendo wanaoshambulia maeneo yanayodhibitiwa na M23.

Kuanzia Jumatatu, tarehe 5 Mei, mapigano makali yalisikika kati ya M23 na Wazalendo katika maeneo ya Katogota Kamanyola na milima ya Rutebe, Kayange na Luzinzi katika Tarafa za Walungu na Uvira.

Kanali Nsabimana Mwendangabo Samuel, afisa wa M23 anayesimamia uhusiano kati ya jeshi na raia, alipokuwa akizungumza na wananchi Ijumaa, alitoa makataa ya wiki moja kwa wapiganaji wa FARDC na Wazalendo walioko Walungu kujisalimisha. Vinginevyo, M23 itawashambulia vikali.

Akasema:

“Vijana wa Walungu, nataka niwaambie jambo moja. Tumekuja kama jeshi lililofunzwa vizuri. Hao watu tutawafanya somo. Tunawapa wiki moja tu waondoke. Nzimbila tutawakamata na kuwapiga, Shabunda tutawachapa, Kingurube na kule Lubira watakiona.”

Kanali Nsabimana alisisitiza kuwa kama hawatatia silaha chini, M23 itawawinda na kuwapa adhabu kali.

Sangiza iyi nkuru

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *