99543857-0-image-a-6_1750355020779

Manchester City Yatozwa Faini ya Pauni Milioni 1 kwa Kuvunja Sheria za Premier League Mara Tisa

Klabu ya Manchester City imetozwa faini ya pauni milioni 1 baada ya kukiri kuvunja sheria za Ligi Kuu ya England mara tisa katika msimu wa 2024/2025.

Makosa haya yanahusiana na kuchelewa kuanza mechi au kipindi cha pili cha mchezo, kinyume na kifungu cha L.33 cha kanuni za Premier League.

Premier League ilitangaza kuwa makosa hayo yalifanyika katika mechi tisa, ikiwemo ile iliyochezwa kwenye Uwanja wa Etihad ambapo City ilifungwa 2-1 na Manchester United mwezi Desemba 2024.

City ilitozwa faini ya pauni 40,000 kwa kosa la kwanza, na kiwango hicho kiliongezeka hadi kufikia pauni 190,000 kwa kosa la tisa.

Klabu hiyo iliitaarifu Premier League kuwa tayari imeomba radhi na kuwakumbusha wachezaji na benchi la ufundi umuhimu wa kufuata sheria za ligi.

Si mara ya kwanza kwa Manchester City kuadhibiwa kwa kuchelewa; msimu wa 2023/2024, walitozwa faini ya pauni milioni 2.09 kwa makosa sawa yaliyofanyika mara 22.

Hii inatokea wakati ambapo Manchester City bado inakabiliwa na kesi kubwa ya madai ya kuvunja sheria 130 za Matumizi Sahihi ya Fedha (Financial Fair Play) kati ya mwaka 2009 hadi 2018. Iwapo watapatikana na hatia, klabu hiyo inaweza kupewa adhabu kali ikiwemo kushushwa daraja kutoka Premier League.

Sangiza iyi nkuru

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *