GridArt_20250704_114609145

Marais Watano wa Afrika Kutua Washington kwa Mazungumzo na Donald Trump

Marais watano wa nchi za Afrika wanatarajiwa mjini Washington, Marekani, kwa mkutano wa ngazi ya juu na Rais Donald Trump, utakaoanza tarehe 9 hadi 11 Julai.

Viongozi hao ni:

  • Jenerali Clotaire Brice Oligui Nguema – Rais wa Gabon

  • Bassirou Diomaye Faye – Rais wa Senegal

  • Joseph Boakai – Rais wa Liberia

  • Mohamed Ould Ghazouani – Rais wa Mauritania

  • Umaro Mokhtar Sissoco Embaló – Rais wa Guinea-Bissau

Trump anapanga kuwakaribisha marais hao katika chakula cha jioni White House tarehe 9 Julai, ambapo pia kutafanyika mazungumzo ya pande mbili na ya pamoja.

Ripoti zinaonyesha kuwa utawala wa Trump unalenga kuimarisha ushirikiano na Afrika, hasa katika nyanja za biashara na madini ya thamani.

Afisa mmoja kutoka White House alisema kuwa Trump anaamini:

“Nchi za Afrika zinatoa fursa za kipekee za kibiashara ambazo zinaweza kufaidisha Wamarekani na washirika wao wa Afrika.”

Mazungumzo hayo yatajikita zaidi katika jinsi Marekani inaweza kupata madini muhimu kama lithium, cobalt, na madini adimu duniani (rare earths), yanayotumika sana katika viwanda vya kielektroniki na nishati mbadala.

Sangiza iyi nkuru

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *