FotoJet-38-768x432_copy_1000x600

Marekani Yaitaka Tanzania Kufafanua Kukamatwa kwa Wanaharakati

Marekani imeiomba Tanzania maelezo na kutaka uchunguzi ufanyike kuhusiana na kukamatwa na kufukuzwa kwa wanaharakati wawili – mmoja kutoka Kenya na mwingine kutoka Uganda – waliokuwa wakizuiliwa ndani ya ardhi ya Tanzania.

Mnamo Ijumaa tarehe 23 Mei, ilibainika kuwa Boniface Mwangi na mwandishi wa habari Agather Atuhaire walitupwa mipakani mwa nchi walikotoka baada ya kuzuiliwa kwa saa kadhaa katika sehemu isiyojulikana.

Wawili hao walikamatwa walipokuwa wamefika Tanzania kuhudhuria kesi ya mwanasiasa wa upinzani Tundu Lissu.

Idara ya Mambo ya Afrika ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilieleza wasiwasi mkubwa kuhusu “unyanyasaji wa wanaharakati wa Afrika Mashariki waliokamatwa nchini Tanzania.”

Mwangi na Atuhaire walisema walipitia mateso wakati wa kuzuiliwa kwao.

Marekani iliongeza:

“Tunataka uchunguzi wa haraka na wa kina kuhusu madai ya ukiukaji wa haki za binadamu. Tunazitaka nchi zote za eneo hili kuwawajibisha wale wote wanaohusika na mateso na uvunjaji wa haki za binadamu.”

Mbali na Marekani, shirika la kimataifa la Amnesty International pia lilitoa wito Ijumaa kwa Tanzania kufanya uchunguzi kuhusu madai ya mateso dhidi ya wanaharakati hao.

Tanzania inazidi kukabiliwa na presha, hasa baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kutoa onyo kuwa serikali yake haitavumilia mtu yeyote atakayejihusisha na kuingilia mambo ya ndani ya nchi hiyo.

Sangiza iyi nkuru

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *