Marekani imesitisha usafirishaji wa silaha fulani kwenda kwa Ukraine ambazo ziliahidiwa wakati wa utawala wa Joe Biden, huku Urusi ikiongeza mashambulizi dhidi ya Ukraine.
Miongoni mwa silaha zilizoahidiwa ni pamoja na zile za kuimarisha ulinzi wa Ukraine, ambazo sasa ziko chini ya uchunguzi mpya baada ya Pentagon kutathmini upya hifadhi ya silaha za Marekani.
Uamuzi huu unaweza kuashiria mabadiliko ya vipaumbele chini ya utawala mpya wa Rais Donald Trump, kwa mujibu wa taarifa kutoka Al Jazeera.
Jumanne, msemaji wa Ikulu ya White House, Anna Kelly, alisema:
“Uamuzi huu umechukuliwa kwa lengo la kuweka maslahi ya Marekani mbele, baada ya kutathmini upya misaada ya kijeshi tunayotoa kwa mataifa mbalimbali duniani.”
Tathmini ya ndani iliyofanywa na Wizara ya Ulinzi ya Marekani ilibaini kuwa baadhi ya maghala ya silaha yako katika viwango vya chini sana, hivyo haiwezekani kuharakisha upelekwaji wa silaha kwa Ukraine, alisema afisa mmoja wa Marekani ambaye hakutaka kutajwa jina lake, kama ilivyoripotiwa kwanza na Politico.
Msemaji wa Pentagon, Sean Parnell, alisema:
“Jeshi la Marekani halijawahi kuwa tayari na lenye uwezo mkubwa kama sasa.”
Kwa mujibu wa Politico na vyombo vingine vya habari Marekani, silaha zilizositishwa ni pamoja na:
Makombora ya ulinzi wa anga ya Patriot
Silaha za kisasa za masafa marefu (precision artillery)
Makombora ya Hellfire




