Chama cha Leadership and Governance for Development (LGD) kinasema kuwa kiongozi wake katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Augustin Matata Ponyo, ametoweka.
Matata Ponyo aliwahi kuwa Waziri Mkuu wa DRC kuanzia mwaka 2012 hadi 2017, chini ya utawala wa Joseph Kabila.
Katika taarifa iliyotolewa siku ya Jumamosi, tarehe 31 Mei, chama chake kilitangaza kuwa alitoweka siku moja baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 10 cha kazi ya lazima.
Adhabu hiyo ilitolewa na Mahakama ya Katiba, baada ya Matata Ponyo kupatikana na hatia ya kufuja dola milioni 245, zilizotengwa kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa eneo la viwanda vya kilimo katika Bukanga-Lonzo.
Chama chake kinasema hawajui aliko, huku taarifa nyingine zikidai kuwa huenda alikimbilia Ubelgiji, baada ya kutoroka kupitia Brazzaville.




