78341

Mechi ya Amani: Jeshi la Rwanda na Uganda Kukutana Uwanjani

Jumamosi hii, tarehe 31 Mei 2025, kikosi cha RDF (Jeshi la Ulinzi la Rwanda) kutoka Divisheni ya Tano ya Vikosi vya Ardhi kitapambana na kikosi cha UPDF (Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Uganda) cha Divisheni ya Pili kwenye uwanja wa Kyamate, mjini Ntungamo, mashariki mwa Uganda, katika mchezo wa kirafiki wa kandanda.

Mchezo huu ni sehemu ya mpango uitwao Proximity Commanders’ Engagements, unaolenga kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya majeshi ya nchi hizi mbili, hasa katika kushughulikia changamoto za kiusalama zinazovuka mipaka na za kikanda.

Ujumbe wa jeshi la Rwanda utapokelewa rasmi na Meja Jenerali Paul Muhanguzi, kamanda wa Divisheni ya Pili ya UPDF, pamoja na maafisa wengine waandamizi wa jeshi la Uganda.

Mchezo huu utakuwa wazi kwa wananchi wote, kama ishara ya mshikamano kati ya jeshi na raia.

Mbali na mechi, wanajeshi wa nchi zote mbili kwa kushirikiana na viongozi wa mitaa watafanya shughuli kama vile mathafara kuelekea mjini Ntungamo, upandaji miti, na uchangiaji damu, kwa lengo la kuendeleza ushirikiano kati ya wanajeshi na raia.

Sangiza iyi nkuru

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *