GridArt_20250529_100157486

Mukwege Asema Wazi: “Kabila Anatumika na Rwanda”

Daktari na mwanasiasa wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Dkt. Denis Mukwege, amesisitiza madai ya serikali ya Kinshasa kwamba Rais wa zamani Joseph Kabila Kabange anatumika na Rwanda.

Kabila, ambaye aliongoza DRC kati ya mwaka 2001 hadi 2019, amekuwa akituhumiwa kwa muda mrefu na serikali ya Congo kwa kushirikiana na kundi la waasi la M23, ambalo Kinshasa inasema linaungwa mkono na Rwanda.

Madai hayo yamekuwa makali zaidi hivi karibuni baada ya Kabila kutangaza kuwa ana mpango wa kuelekea maeneo ya mashariki mwa DRC yanayodhibitiwa na kundi hilo.

Tangu Jumapili iliyopita, Kabila amekuwa katika jiji la Goma, linalodhibitiwa na M23. Habari zinasema kuwa akiwa huko, amekutana na viongozi wa muungano wa AFC ambao unajumuisha kundi la M23.

Katika mahojiano aliyofanya hivi karibuni na France 24, Dkt. Mukwege naye amethibitisha madai ya Kinshasa kwamba Kabila anatumika na Rwanda.

Alipoulizwa na mwandishi Marc Perelman iwapo anaamini kuwa Kabila ni “kibaraka wa Rais Paul Kagame”, Mukwege alijibu:

“Hotuba zake zinaeleza kila kitu. Hajawahi kumlaumu Rais wa Rwanda kama mvamizi [wa DRC], ingawa Azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa namba 2773 linaamuru Rwanda kuondoka DRC bila masharti. Zaidi ya hayo, aliingia [Goma] kupitia Rwanda. Hayo ni mambo yasiyopingika. Naweza kusema kuwa matendo yake sasa yanaonekana wazi.”

Mukwege pia alisema kwamba Kabila anapaswa kueleza kwa watu wa Congo kwa nini, mwaka 2018, aliamua kumpa uongozi Félix Antoine Tshisekedi, licha ya kwamba hakuwa mshindi halali wa uchaguzi huo.

Sangiza iyi nkuru

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *