President-Museveni-addressing-guests-during-the-commissioning-ceremony-for-cardets-at-Kaweweta-on-Tuesday.-PPU-photoPIX1-scaled

Museveni Alidanganywa? Kiongozi wa ADF Meddie Nkalubo Aripotiwa Kuwa Hai Miaka Miwili Baada ya Kuutangazwa Kufariki

Miaka miwili baada ya Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni kutangaza kuwa jeshi la nchi hiyo lilimuua kiongozi wa kundi la kigaidi la ADF, Meddie Nkalubo, sasa imebainika kuwa bado yuko hai.

Mnamo Septemba 2023, Museveni alitangaza kupitia runinga ya taifa kuwa majeshi ya Uganda yalimuua Nkalubo kupitia shambulio la anga dhidi ya kambi za ADF huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). Taarifa hizo zilikuwa zimetolewa na Meja Jenerali James Birungi, aliyekuwa mkuu wa ujasusi wa kijeshi wakati huo.

Hata hivyo, baada ya miaka miwili, imegundulika kuwa Meddie Nkalubo hakuuwawa.

Ukweli huu ulifichuka baada ya kukamatwa kwa Sheikh Hamza Lyavala, anayetuhumiwa kushirikiana kwa karibu na ADF na kuwapa maafisa wa usalama wa Uganda taarifa za uongo kuhusu kundi hilo.

Sheikh Lyavala alikamatwa na jeshi la Uganda, akituhumiwa kutoa ujasusi wa kughushi.

Afisa mmoja wa usalama wa Uganda alisema kwamba Lyavala alikuwa amejijengea imani kubwa miongoni mwa idara za ujasusi kwa kuwapa mara kwa mara taarifa muhimu kuhusu ADF ambazo ni vigumu kupatikana.

Hata hivyo, ilibainika kuwa Lyavala alitumia uaminifu huo kuwapotosha maafisa wa ujasusi na wale wa kupambana na ugaidi kwa kuwapa taarifa za uongo, ikiwemo madai ambayo yalimfanya Rais Museveni kutangaza kwa makosa kuwa Nkalubo ameuawa.

Ripoti zinasema kuwa baada ya tangazo hilo la Museveni, ilithibitishwa kuwa Meddie Nkalubo alikuwa bado hai na alikuwa anaendelea kuongoza mashambulizi ya kigaidi ya ADF mashariki mwa DRC.

Wakati wa kukamatwa kwa Lyavala, jeshi la Uganda lilimshutumu kwa kushirikiana na Nkalubo kupotosha idara za ujasusi kuhusu kuuawa kwake.

Sangiza iyi nkuru

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *