9557cc00-dee9-11ef-a819-277e390a7a08.jpg

Mwanaume Aliyewasha Moto Kurani Apigwa Risasi na Kufa.

Salwan Momika, mwanaume mwenye umri wa miaka 38 aliyejulikana baada ya kuwasha moto Kurani, amepigwa risasi na kuuawa nchini Sweden, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya huko.

Mwanamme huyu wa asili ya Iraq aliyekuwa akiishi Sweden alipigwa risasi jioni ya Jumatano nyumbani kwake Södertälje, karibu na Stockholm.

Polisi iliripoti kuwa watu watano walikamatwa baada ya tukio la kupigwa risasi kwa mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 40.

Momika alijulikana sana kutokana na maandamano aliyofanya mwaka 2023, ambapo aliwasha moto Kurani karibu na misikiti, jambo lililosababisha hali ya sintofahamu na maandamano katika nchi nyingi zenye Waislamu wengi.

Mwezi Agosti 2023, Momika alishtakiwa pamoja na mtu mwingine kwa kosa la “kudhalilisha kundi la watu” mara nne tofauti.

Mahakama ya Stockholm ilikuwa imepanga kutoa hukumu siku ya Alhamisi lakini ilitangaza kuahirisha kesi hiyo baada ya kuthibitisha kifo chake.

Sweden hapo awali ilimruhusu Momika kuwasha moto Kurani kwa misingi ya sheria za uhuru wa kujieleza, lakini baadaye ilitangaza kuwa itazingatia kuweka vizuizi kwa maandamano ya aina hiyo katika mazingira fulani.

Sangiza iyi nkuru

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *