Mwanaume mwenye umri wa miaka 68 kutoka Afrika Kusini alipatikana amefariki bafuni kwake asubuhi ya Jumatano, Mei 7, katika eneo la Parklands, jijini Nairobi, Kenya.
Polisi walisema uchunguzi wa awali ulionyesha kuwa Mark Nalon Minter aliwasili nchini tarehe 1 Mei kwa safari ya kikazi na alitarajiwa kuondoka Mei 10.
Alikuwa na mwanamke mwenzake wakati tukio lilipotokea. Mwanamke huyo aliwaambia polisi kuwa walikuwa wamelala baada ya chakula cha jioni, lakini alipoamka asubuhi ya Jumatano, hakumuona.
Baadaye alimkuta amelala bila kusonga bafuni, ambapo inaaminika alianguka. Kwa mujibu wa tovuti ya habari ya The Star nchini Kenya, alikumbwa na mauti hapo.
Wahudumu wa St John walifika, lakini baada ya kumchunguza walithibitisha kuwa tayari alikuwa amekufa.
Dawa mbalimbali za kutibu shinikizo la damu na kisukari zilipatikana kwenye begi lake.
Polisi wameanzisha uchunguzi wa kina kuhusu kifo hicho.




