Idara ya Usalama wa Ndani ya Marekani (DHS) imetangaza kuwa Idara ya Uhamiaji na Forodha (ICE) imemkamata raia wa Mexico anayeshukiwa kupanga njama ya kumpiga risasi Rais wa zamani Donald Trump.
DHS, kupitia kwa Katibu wake Kristi Noem, ilitoa taarifa ya kupongeza maafisa wa uhamiaji kwa kumkamata mshukiwa ambaye hakuwa na hati halali za kusafiria, na kwa sasa yuko mikononi mwa vyombo vya sheria.
Mshukiwa huyo, Ramon Morales Reyes, mwenye umri wa miaka 54, aliripotiwa kuandika barua kwa mkono wake mapema mwezi huu, akieleza dhamira yake ya kumpiga risasi Donald Trump iwapo angemwona katika kampeni zake.
Mwanaume huyo mwenye asili ya Mexico anailaumu Marekani kwa kuwafukuza wanafamilia wake.
Akaandika:
“Tumechoshwa na Rais huyu anayetudharau sisi Wameksiko. Tumefanya mengi kwa nchi hii kuliko ninyi Weupe.”
Morales anaripotiwa kuwa aliingia Marekani kinyume cha sheria angalau mara tisa kati ya mwaka 1998 na 2005, na ana historia ya makosa ya jinai, ikiwemo tukio la kugonga mtu hadi kufa na kutoroka.
Baada ya kukamatwa kwake, mamlaka za Marekani zinajiandaa kumrudisha Mexico.




