Mwigizaji wa filamu kutoka Rwanda, Natacha Ndahiro, amesema hana tatizo lolote la kuigiza katika filamu zenye maudhui ya mapenzi au ngono ikiwa ni kwa ajili ya maendeleo ya kazi yake katika sanaa ya uigizaji.
Katika mahojiano na IGIHE, Natacha alisema kuwa uigizaji ni kazi kama kazi nyingine, na marafiki na familia yake wanafahamu hilo. “Wanaonizunguka wanajua ni kazi. Tunachofanya kinaonekana pia kwenye filamu za kimataifa,” alisema.
Alieleza kuwa hana pingamizi kuigiza sehemu za busu au mapenzi alimradi ni kwa manufaa ya kazi yake. “Ikiwa ni filamu inayokwenda kuonyeshwa kwenye Netflix na itanisaidia kuendelea, nitafanya kila kinachotakiwa,” aliongeza.
Natacha aliwahimiza Wanyarwanda waelewe kuwa filamu ni kazi, si jambo la aibu, na kuwa hayo yanafanyika pia katika filamu za kimataifa bila matatizo.
Ameshiriki katika filamu nyingi kama Natacha Series, Love is my Sin, Masezerano, Annah, Care na Lover’s Cage, ambayo imezua mjadala mkubwa mitandaoni kwa sababu ya sehemu yenye busu.




