Kijana maarufu kwenye mitandao ya kijamii, hasa TikTok, anayeitwa Umar Hashim na kujulikana kama Tsulange, amehukumiwa na mahakama ya jimbo la Kano, kaskazini mwa Nigeria, kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kosa la kuoga barabarani akiwa amevaa nguo ya ndani ya wanawake.
Mahakama ya Mwanzo ya Gyadi-Gyadi, inayoongozwa na Hadiza Muhammad Hassan, ilimpata na hatia ya tabia isiyofaa hadharani.
Tsulange alipigwa picha akifanya sketch ya ucheshi, ambapo alionekana akioga katikati ya barabara, jambo lililotafsiriwa kama kuvunja maadili ya Kiislamu ya eneo hilo.
Hashim alihukumiwa mwaka mmoja jela, lakini alipewa nafasi ya kulipa faini ya Naira 80,000 (zaidi ya Shilingi 100,000 za Rwanda).
Pia aliagizwa kulipa Naira 20,000 zaidi kugharamia uchunguzi uliofanywa na Kano State Censorship Board, taasisi iliyomfungulia mashitaka mwezi Juni 2025.




