20250529_75202

Pyramids FC yasherehekea ushindi wa Ligi Kuu ya Misri, lakini kombe likakabidhiwa Al Ahly

Timu ya Pyramids FC ilisherehekea kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Misri, ingawa Shirikisho la Soka nchini humo lilikabidhi rasmi kombe hilo kwa wapinzani wao, Al Ahly.

Jumatano jioni, timu zote mbili zilicheza mechi zao za mwisho za mchujo ambazo zilikamilisha msimu wa ligi ya Misri.

Al Ahly waliifunga Pharco FC mabao 6-0, huku Pyramids FC wakiifunga Ceramica Cleopatra mabao 5-1. Matokeo haya yalimfanya Al Ahly kutwaa ubingwa wakiwa na alama 58, wakitangulia Pyramids FC kwa alama mbili.

Hii ilikuwa mara ya 45 kwa Al Ahly kutwaa taji hilo katika historia yao.

Timu zote mbili zilisherehekea kombe hilo!

Wakati Al Ahly walikabidhiwa kombe na kulisherehekea, upande mwingine, wachezaji na makocha wa Pyramids FC nao walishangilia wakisisitiza kuwa wao ndio waliostahili kutangazwa mabingwa — ambao ungekuwa ushindi wao wa kwanza kabisa kihistoria.

Pyramids FC wanadai kuwa walistahili kombe kutokana na mechi ya ligi ambayo Al Ahly walistahili kucheza dhidi ya wapinzani wao Zamalek lakini wakagoma kucheza kwa sababu walitaka mechi hiyo isimamiwe na waamuzi wa kigeni — ombi ambalo halikukubaliwa na waandaaji wa ligi.

Kwa kuwa Zamalek walitimiza masharti yote ya kufanikisha mechi, Al Ahly walipewa sare ya kufungwa 3-0 kwa kushindwa kujitokeza.

Sheria za Misri zinasema kuwa timu inayogoma kucheza mechi inayopaswa kufanyika hukabiliwa na kupoteza 3-0 na kukatwa alama tatu zaidi — jumla ya adhabu ya alama 6.

Kwa mujibu wa sheria hiyo, Al Ahly walipaswa kupoteza alama 6 — tatu kwa kufungwa mechi hiyo na tatu kwa adhabu ya kutoshiriki.

Hilo halikutekelezwa. Al Ahly walikata rufaa wakidai kuwa waandaaji wa ligi walikuwa na makosa kwa kuwakatalia waamuzi wa kigeni wakati walikuwa wamewaruhusu timu nyingine. Hatimaye, Al Ahly walipoteza mechi hiyo kwa 3-0 lakini hawakukatwa alama.

Pyramids FC, waliokuwa kileleni wakati huo, walikata rufaa dhidi ya uamuzi huo lakini wakakataliwa.

Kwa sasa, Pyramids wanasisitiza kuwa sheria iheshimiwe na kwamba wao ndiyo wanaostahili kutangazwa mabingwa — na hiyo ndiyo sababu walisherehekea ushindi wao.

Iwapo Al Ahly wangekatwa alama 3 kama inavyotakiwa, Pyramids FC wangeishia na pointi 56 dhidi ya pointi 55 za Al Ahly.

Hata hivyo, Al Ahly walipewa kombe, licha ya Pyramids kuwasilisha ombi kwa Mahakama ya Kimataifa ya Michezo (CAS) kuzuia utoaji wa kombe hilo. Ombi hilo pia lilikataliwa.

Sangiza iyi nkuru

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *