Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni, amemkaribisha mwinjilisti wa kimataifa kutoka Marekani, Mchungaji Benny Hinn, katika ikulu ya Nakasero, kwenye kikao kilichojaa maombi na mazungumzo ya kiroho kuhusu nafasi ya Ukristo katika maendeleo ya Afrika.
Museveni alisema ujumbe wa Yesu kuhusu upendo na ufufuo umeleta thamani kubwa katika tamaduni za Kiafrika.
Akasema:
“Watu wetu walikuwa tayari wanamjua Mungu—tunamwita Katonda. Lakini ujumbe wa ufufuo ulikuwa mpya na wa thamani sana.”
Kwa upande wake, Mchungaji Benny Hinn alijibu akisema:
“Uhai si kitu, ni mtu — na jina lake ni Yesu.”
Mchungaji Robert Kayanja, aliyeandaa ziara hiyo, alimshukuru Rais Museveni kwa mapokezi ya heshima, kwa kumuhakikishia Mchungaji Hinn ulinzi na vifaa, na pia kwa upendo anaouonesha kwa kanisa na taifa.
Tukio hilo lilihitimishwa kwa maombi yaliyosomwa na Mchungaji Hinn, aliyemuombea familia ya rais pamoja na taifa la Uganda. Pia zawadi zilibadilishanwa kama ishara ya heshima na ushirikiano katika kuendeleza Injili na maendeleo ya taifa.
Mchungaji Benny Hinn yupo katika ziara ya siku tatu jijini Kampala, ambapo alihudhuria ibada kubwa ya pamoja katika kanisa la Miracle Centre Jumamosi na Jumapili.




