InShot_20250531_080636949

Rais Ndayishimiye Amkemea Mkombozi, Msanii Aliyeingia Siasa

Mnamo Ijumaa, Mei 30, 2025, Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye, alitoa matamshi tata kuhusu msanii Mkombozi Lucifer, ambaye hivi karibuni alitangaza azma yake ya kugombea Ubunge, licha ya kufahamu kuwa nafasi yake ya kushinda ni ndogo.

Rais aliyasema haya akiwa Bujumbura, alikokuwa akishiriki na vijana katika kurekebisha uwanja wa michezo wa Campus Kamenge.

Katika hotuba yake, Rais alisema alimwuliza Mkombozi kwa nini aliamua kutumia milioni 2 za faranga za Burundi kuendesha kampeni wakati anajua hatashinda.

Alisema:

“Aliniambia kwamba si hasara kwa sababu hata akikosa kuchaguliwa, pesa hizo zitaingia kwenye hazina ya serikali na kusaidia taifa. Lakini nikamwambia: ‘Kumbuka kuwa siasa si uwanja wa michezo au burudani.'”

Kauli hiyo ya Rais ilizua hisia tofauti mitandaoni, baadhi wakimsifu kwa kusema ukweli, wengine wakimshutumu kwa kujaribu kuzuia haki ya kidemokrasia ya watu kutoka sekta nyingine kuwania nyadhifa za kisiasa.

Mkombozi Lucifer, ambaye alitambulika kupitia muziki, anahitaji angalau asilimia 40 ya kura ili kuruhusiwa kuingia Bungeni.

Haya yanajiri wakati uchaguzi unapokaribia, na mjadala kuhusu uwezo na mienendo ya wagombea unazidi kushika kasi nchini Burundi.

Sangiza iyi nkuru

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *