20250528_125406

Rais Ndayishimiye Asema: “Hatutatoa Madaraka – Tulipigania Kwa Jasho na Damu”

Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye, amewakatia tamaa wale wanaotarajia kwamba chama chake tawala, CNDD-FDD, kitaondoka madarakani, akisema kuwa jambo hilo haliwezekani kwa sababu walikipata kwa shida kubwa.

Katika mkutano wa kampeni wa CNDD-FDD uliofanyika Mei 27, 2025, Ndayishimiye alisema:
“Tulikipata hiki nchi kwa taabu na mateso. Hatuwezi kamwe kukikabidhi kirahisi tulichopigania kwa nguvu zote.”

Katika mkutano huo uliofanyika katika manispaa ya Musigati, Ndayishimiye alisema kuwa kabla ya CNDD-FDD kushika hatamu, Burundi ilikuwa katika machafuko makubwa. Lakini sasa wamelijenga na kulifanya taifa lenye demokrasia.

Aliongeza kuwa Burundi sasa ni salama, linaheshimiwa kimataifa, na kwamba Mburundi popote alipo duniani anaheshimiwa pia.

Licha ya nia ya Rais Ndayishimiye kutaka chama chake kiendelee kutawala, miaka 20 ya uongozi wa CNDD-FDD haijaonesha maendeleo ya kweli. Taifa bado linakabiliwa na changamoto kubwa.

Serikali yake imeshindwa kutatua tatizo la mafuta ambalo limekuwepo kwa zaidi ya miaka mitatu, uhaba wa sukari, kupanda kwa bei za bidhaa muhimu, na uhaba mkubwa wa fedha za kigeni. Haya yote yameendelea kuifanya Burundi kuwa miongoni mwa nchi maskini zaidi duniani.

Sangiza iyi nkuru

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *