20250604_060252

Rwanda na Algeria Wasaini Mikataba 12 Mpya, Ikiwemo Kusafiri Bila Visa

Rwanda na Algeria jana Jumanne walisaini mikataba 12 mipya ya ushirikiano katika sekta muhimu, zikiwemo usafiri wa anga na kuondoa visa.

Sherehe ya kusaini mikataba hiyo ilifanyika baada ya mazungumzo kati ya Rais Paul Kagame na mwenzake wa Algeria, Abdelmadjid Tebboune.

Rais wa Rwanda yuko nchini humo kaskazini mwa Afrika kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.

Ikulu ya Rwanda imetangaza kuwa sekta 12 zilizohusishwa katika mikataba hiyo ni pamoja na usafiri wa anga, kuondoa visa, mawasiliano, polisi, viwanda vya dawa, elimu ya juu, haki, ukuzaji wa uwekezaji, na ujasiriamali.

Mikataba hiyo mipya inaongeza kwenye ile ambayo tayari ipo kati ya Kigali na Algiers katika elimu, jeshi na usalama.

Mbali na mazungumzo na kusaini mikataba hiyo, Marais Kagame na Tebboune pia walifanya mkutano wa pamoja na waandishi wa habari.

Katika mkutano huo, Rais Kagame alithibitisha kuwa Rwanda itafungua Ubalozi nchini Algeria katika siku zijazo.

Pia, Rais Kagame alitembelea na kuweka shada la maua katika Mnara wa Maqam Echahid, kwa heshima ya mashujaa wa Algeria waliopoteza maisha yao katika vita vya kupigania uhuru wa nchi hiyo.

Sangiza iyi nkuru

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *