bnr1

Rwanda Yaweza Kuingiza Bidhaa kwa Miezi 4.7 Bila Kukopa – BNR Yapanga Kuhifadhi Dhahabu

Benki Kuu ya Rwanda (BNR) imetangaza kuwa nchi ina akiba ya kutosha ya dola za Marekani ambayo inaweza kutumika kuagiza bidhaa zote zinazohitajika kwa kipindi cha miezi 4.7, bila kuhitaji fedha za ziada kutoka nje. Aidha, Rwanda ipo mbioni kuanza kuwekeza kwenye dhahabu kama sehemu ya akiba ya taifa.

BNR imesema kuwa Rwanda inaanza kuwekeza kwenye dhahabu, itakayotumika kama akiba rasmi ya fedha za kigeni – kama ilivyozoeleka kutumia dola za Marekani. Hatua hii inalenga kuimarisha misingi ya uchumi wa taifa na kuongeza ustahimilivu wa kiuchumi dhidi ya mabadiliko ya kisiasa na kibiashara duniani.

Gavana wa BNR, Soraya Hakuziyaremye, amesema kuwa mpango huu wa dhahabu ni miongoni mwa mikakati ya benki hiyo ya kuhakikisha ustawi wa kiuchumi kwa muda mrefu.

Wachambuzi wa masuala ya uchumi wamepongeza hatua hiyo, wakieleza kuwa mataifa mengi duniani yanageukia dhahabu kama njia ya kujikinga dhidi ya misukosuko ya kisiasa na kibiashara ya kimataifa. Hata hivyo, wanasema si busara kuiweka asilimia 100 ya akiba ya taifa kwenye dhahabu pekee.

Akiba ya dhahabu ita ongeza nguvu kwa akiba ya sasa ya dola.
Hadi sasa, kiasi halisi cha uwekezaji kwenye dhahabu hakijatangazwa.

Sangiza iyi nkuru

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *