Jumatatu, tarehe 16 Juni, kikao cha pamoja cha Seneti ya Rwanda kiliidhinisha maoni yake kuhusu bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha wa 2025/2026, ikionesha kuridhika kuwa mapendekezo ya Maseneta yalizingatiwa, hasa kuongezwa kwa bajeti ya sekta ya kilimo.
Seneti pia ilisifu ongezeko la fedha katika sekta nyingine kulingana na mapendekezo yake ya awali, ikiwemo:
Kuongeza bajeti ya nishati, ili kufanikisha lengo la umeme kwa wote;
Kuongeza bajeti kwa wilaya za Nyamagabe, Gisagara, Rutsiro, Kamonyi, Karongi na Kayonza, kusaidia kupunguza umasikini;
Hatua za kuwezesha sekta binafsi na kuunda ajira kwa vijana;
Fedha za kujenga, kukarabati na kuunganisha makumbusho ya Mauaji ya Kimbari dhidi ya Watutsi.




