GuBzPwLXcAAXuXS

Shambulio la Kijitoa Muhanga Lagonga Mwamba Tena Kampala – Mwanamke Apigwa Risasi

Vyombo vya usalama vya Uganda vimefyatua risasi na kumuua mwanamke wa pili aliyekuwa akishukiwa kujaribu kutekeleza shambulio la kujitoa muhanga jijini Kampala, baada ya jaribio lingine kushindikana hivi karibuni huko Munyonyo.

Kulingana na taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa X na Jeshi la Ulinzi la Uganda (UPDF), mshukiwa huyo aliuawa katika soko la Kalerwe, eneo lenye msongamano mkubwa kaskazini mwa Kampala. UPDF ilithibitisha kuwa “kikosi cha mabomu” kilitumwa kuchunguza na kulinda eneo hilo.

Picha iliyoambatana na taarifa hiyo inaonyesha mshukiwa akiwa amelala chini karibu na pikipiki na begi jeusi la safari, linalodhaniwa kuwa lilikuwa na vilipuzi.

Tukio hili linatokea wiki chache baada ya shambulio lingine la kigaidi kuzuiwa huko Munyonyo, ambapo mshambuliaji wa kujitoa muhanga aliyekuwa amevaa koti lenye bomu alikamatwa na kikosi maalum cha UPDF alipokuwa akielekea kwenye Basilika ya Munyonyo.

Sangiza iyi nkuru

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *