IMG_4070_1751968208

Trump Arejesha Msaada wa Silaha kwa Ukraine Baada ya Kusitishwa

Rais wa Marekani, Donald Trump, ametangaza kuwa serikali yake itarudisha msaada wa silaha kwa Ukraine, baada ya kusitisha baadhi ya msaada wa kijeshi hapo awali.

Alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na wanahabari kabla ya chakula cha jioni na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu.

Trump alisema:

“Tutawapatia tena vifaa. Wanapaswa kujilinda. Wanashambuliwa kwa nguvu sana.”

Hii inajiri baada ya Ikulu ya White House kusema kuwa kusitishwa kwa msaada huo kulikuwa kwa lengo la kufanya tathmini ya jinsi fedha za Marekani zinavyotumika kusaidia mataifa ya nje, kwa kuzingatia masilahi ya Marekani.

Marekani imeeleza kuwa katika mwelekeo mpya wa Trump, Ukraine itapokea tena vifaa vya kijeshi, ikiwemo silaha za ulinzi wa anga, kusaidia nchi hiyo kujilinda.

Sangiza iyi nkuru

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *