InShot_20250605_120113435

Ubelgiji Wathibitisha Kushiriki! Rwanda Yakaribisha kwa Furaha Mashindano ya Dunia ya Baiskeli 2025

Waziri wa Mambo ya Nje, Balozi Olivier Nduhungirehe, amepongeza uamuzi wa Shirikisho la Baiskeli la Ubelgiji ambalo limethibitisha kuwa litashiriki katika Mashindano ya Dunia ya Baiskeli ya 2025 yatakayofanyika Kigali kuanzia tarehe 21 hadi 28 Septemba 2025.

Uamuzi huu umetolewa wakati ambapo uhusiano wa kidiplomasia kati ya Rwanda na Ubelgiji si mzuri. Mnamo Machi 2025, Serikali ya Rwanda ilisitisha uhusiano wa kidiplomasia na Ubelgiji na kuwaamuru wanadiplomasia wake kuondoka nchini.

Hata hivyo, Ubelgiji imethibitisha kuwa itashiriki katika mashindano haya makubwa ya kimataifa ya baiskeli, ambayo kwa mara ya kwanza yatafanyika barani Afrika — jambo linaloweza kufungua ukurasa mpya wa ushirikiano wa michezo kati ya mataifa haya mawili.

Kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter), Balozi Olivier Nduhungirehe alisema:

“Uamuzi mzuri na unaoelekea mwelekeo sahihi. Timu ya baiskeli ya Ubelgiji inakaribishwa Rwanda, kama zilivyo timu zote zitakazoshiriki.”

Akaongeza:

“Mashindano ya Dunia ya Baiskeli yatafanyika Rwanda kuanzia Septemba 21 hadi 28, 2025. Yatakua ya kwanza kufanyika Afrika. Lazima yawe sherehe ya michezo na furaha kwa wananchi wote.”

Kauli hizi zilitolewa baada ya taarifa kutoka gazeti la Sporza la Ubelgiji kuripoti kwamba Shirikisho la Baiskeli la Ubelgiji (Belgian Cycling) limeamua rasmi kushiriki mashindano hayo, kama ilivyothibitishwa na Mkurugenzi Mkuu wake, Nathalie.

Rwanda inaendelea na maandalizi kwa ajili ya mashindano haya ya kimataifa yatakayowaleta pamoja wakali wa baiskeli duniani, na ambayo yanatarajiwa kukuza utalii na kuitangaza nchi kimataifa.

Sangiza iyi nkuru

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *