©PHOTOPQR/LE PARISIEN / JEROME Benjamin -  COURCOURONNES LE 12 03 2012 - AGATHE HABYARIMANA 
VEUVE DU PRESIDENT RWANDAIS TUE DANS L ATTENTAT DE SON AVION EN AVRIL 1994
ICI DANS SA MAISON DE COURCOURONNES
widow of the Rwanda President dead in his airplane attack in april 1994
Here : in his house in Courcouronnes (MaxPPP TagID: maxnewsworldthree146817.jpg) [Photo via MaxPPP]

Ufaransa: Agathe Habyarimana Hatashtakiwa – Uchunguzi Wafungwa Bila Mashtaka

Uchunguzi uliokuwa ukiendeshwa nchini Ufaransa dhidi ya Agathe Habyarimana, mjane wa aliyekuwa Rais wa Rwanda, Juvénal Habyarimana, umefungwa bila mashitaka yoyote kufunguliwa.

Uamuzi huu ulifanyika Ijumaa, tarehe 16 Mei 2025, kwa mujibu wa vyanzo vya karibu na kesi hiyo.

Majaji walihitimisha kuwa ushahidi uliokuwa ukimhusisha na mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi mwaka 1994 ulikuwa “unapingana, hauna mshikamano, na wa kupotosha.”

Katika uamuzi wao wa Ijumaa, majaji wa uchunguzi walieleza kuwa: “Kwa hatua hii, hakuna ushahidi wa kutosha wala thabiti unaoonyesha kuwa Agathe Habyarimana alihusika kama mshirika katika vitendo vya mauaji ya kimbari […]. Hata kama uvumi unaendelea, kama majaji walivyoeleza, haviwezi kuchukuliwa kama ushahidi iwapo hakuna hoja madhubuti zinazounga mkono.”

Kwa mujibu wa ripoti hii ya RFI, Agathe Habyarimana hajawahi kutoa kauli za hadharani zinazochochea chuki au kuhamasisha mauaji ya kimbari.

Hivyo basi, uchunguzi umefungwa rasmi bila Agathe kushitakiwa kwa kosa lolote.

Agathe Habyarimana mwenye umri wa miaka 82, alikuwa chini ya uchunguzi nchini Ufaransa tangu mwaka 2008 kwa tuhuma za kushiriki mauaji ya kimbari na uhalifu dhidi ya binadamu, lakini hadi sasa hakuna ushahidi wa kuanzisha mashtaka rasmi.

Uchunguzi huu ulianzishwa kufuatia malalamiko ya shirika la “Collectif des parties civiles pour le Rwanda”.

Hata hivyo, uamuzi huu umetolewa wakati ambapo Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Kitaifa wa Ufaransa anayeshughulikia masuala ya ugaidi, iliyokuwa na mamlaka juu ya kesi hii, iliwasilisha hoja zake katika chumba cha uchunguzi cha Mahakama ya Rufaa ya Paris mwezi Septemba 2024, ikiomba Agathe afunguliwe mashtaka.

Kikao cha kusikiliza ombi hilo kinatarajiwa kufanyika Jumatano, tarehe 21 Mei.

Wakili anayewakilisha Shirika la Kimataifa la Haki za Binadamu (FIDH) alielezea masikitiko yake kuhusu kukosekana kwa mashtaka, licha ya kwamba kwa mtazamo wake, kulikuwepo na ushahidi wa kutosha dhidi ya Agathe Kanziga Habyarimana.

Sangiza iyi nkuru

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *