Maafisa wanasema kuwa kubadilishana wafungwa kati ya Ukraine na Urusi kunatarajiwa kuwa kwa kiwango kikubwa zaidi tangu vita kuanza zaidi ya miaka mitatu iliyopita, na kutaendelea siku ya Jumapili.
Katika mazungumzo yaliyofanyika mapema mwezi huu mjini Istanbul, Uturuki, Kyiv na Moscow walikubaliana kubadilishana watu 1,000, wakiwemo wafungwa wa vita na raia waliokamatwa.
Mnamo Jumamosi, tarehe 24 Mei 2025, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy pamoja na Wizara ya Ulinzi ya Urusi walithibitisha kuwa wanajeshi 307 walibadilishanwa, baada ya wanajeshi na raia 390 kuachiliwa siku ya Ijumaa.
Zelenskyy aliandika kupitia ukurasa wake wa Telegram Jumamosi:
“Tunatarajia wengine kesho.”
Hadi sasa, hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa kuhusu idadi ya wafungwa wanaoweza kubadilishanwa siku ya Jumapili, kulingana na ripoti hii ya DW.




