af046940-2d79-11f0-8f57-b7237f6a66e6

Vita kati ya India na Pakistan Yazidi Kuchacha: Makombora, Drones na Mashambulizi ya Kulipiza Kisasi

Baada ya siku chache tu India kuzindua operesheni ya kijeshi iitwayo “Operation Sindoor”, mzozo kati yake na Pakistan umeingia hatua mpya ya hatari.

Usiku wa Mei 11, India ilishambulia kambi tatu za jeshi la anga la Pakistan kwa kutumia makombora ya ardhini kwenda angani. Pakistan imeripoti kuwa watu 13 wamefariki na wengine zaidi ya 50 wamejeruhiwa, wengi wakiwa kutoka eneo la Kashmir.

Pakistan ilijibu kwa kuanzisha operesheni yake iitwayo “Operation Bunyan Marsoos”, ikilenga miundombinu ya kijeshi ya India.

Waziri Mkuu wa Pakistan, Shehbaz Sharif, alitangaza kuwa jeshi la nchi hiyo “limejibu mashambulizi ya India kwa nguvu na kwa mpango mahsusi leo.”

Jeshi la India, siku ya Jumamosi, lilithibitisha kuwa Pakistan ilirusha drones na silaha zingine kwenye ardhi ya India, lakini likasisitiza kuwa mashambulizi hayo yalizimwa.

India pia ilisema kuwa drones nyingi za adui zilionekana juu ya jiji takatifu la Amritsar katika jimbo la Punjab na zilibamizwa hewani.

Ingawa India na Pakistan wamekuwa na mvutano wa muda mrefu, hali ilizidi kuwa mbaya baada ya watalii 26 wa India kuuawa katika shambulio la Kashmir, ambalo India inalaumu Pakistan.

Sangiza iyi nkuru

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *