F2g78weWoAAmnSJ.jpg-20230804101007000000

Wanafamilia 9 wa Rais Tshisekedi Wafikishwa Mahakamani Ubelgiji kwa Kula Njama ya Kupora Madini ya Congo

Watu tisa wa familia ya Rais Félix Antoine Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wamefikishwa mahakamani mjini Brussels, Ubelgiji, wakituhumiwa kupora madini kutoka mikoa ya Haut-Katanga na Lualaba.

Kwa mujibu wa gazeti la Ubelgiji la La Libre, waliofikishwa mahakamani ni pamoja na dada zake, ndugu wa damu, wanawe, kaka zake na mkewe, Denise Nyakeru Tshisekedi.

Wanatuhumiwa kuwa washirika na wanufaika wa ufisadi na vitendo vingine vya uhalifu wa kiuchumi.

Shtaka hilo liliwasilishwa kwa Naibu Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Ubelgiji, Ann Fransen, siku ya Jumanne, Julai 8.

Malalamiko hayo yaliwasilishwa na mawakili Bernard na Brieuc Maingain, kwa niaba ya mashirika kadhaa yasiyo ya kiserikali kutoka mkoa wa Katanga, pamoja na viongozi wanne wa zamani wa kampuni ya madini ya serikali ya Gécamines.

Katika malalamiko yao, mawakili walisema kuwa wanafamilia wa Tshisekedi si wao pekee waliopora madini ya Katanga.

Shtaka hilo lililowasilishwa Brussels linawalenga wale wenye uraia wa Ubelgiji, kwa kuwa mahakama za Ubelgiji zina mamlaka ya kuwashtaki.

Mmoja wa walalamikaji alisema:

“Mashitaka zaidi yanaweza kuwasilishwa katika nchi nyingine ambako waporaji wa utajiri wetu wanatoka.”

Sangiza iyi nkuru

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *