Screenshot_20250701-1917252

Wapinzani wa Burundi Walio Uhamishoni Watangaza Mapambano ya Kivita Dhidi ya Serikali ya Gitega

Baadhi ya wakimbizi wa Burundi walioko Ubelgiji, wakiwemo wanasiasa mashuhuri, wametangaza kuwa watachukua silaha kupambana na serikali ya nchi yao inayoongozwa na chama cha CNDD-FDD. Wanasema njia zote za amani walizojaribu zimeshindwa kutokana na kupuuzwa na serikali.

Walioitoa taarifa hiyo ni pamoja na vyama vya upinzani kama CFOR-Arusha, CNR Ingeri Yarugamba, na MAP Burundi Buhire ambavyo vyote vinafanya kazi uhamishoni na vinampinga Rais Evariste Ndayishimiye.

Katika mkutano uliofanyika hivi karibuni huko Brussels, Ubelgiji, viongozi wa vyama hivyo walidai kuwa uchaguzi wa mwisho ulikuwa na wizi mkubwa na hali ya maisha ya wananchi wa Burundi ni mbaya sana.

Kiongozi mmoja wa harakati hizo mpya za upinzani ni Frederic Bamvuginyumvira, aliyewahi kuwa Makamu wa Rais wa Burundi kuanzia 1998 hadi 2001, na sasa ni Rais wa CFOR-Arusha. Aliliambia vyombo vya habari kuwa wameamua kuchukua silaha ili kupambana na serikali waliyoitaja kuwa imefaili kuongoza.

Alisema:

“Tukitazama hali ilivyo, hakuna sababu ya mtu kusema tusichukue silaha. Serikali hii haikubali hata kidogo sauti tofauti.”

Alieleza kuwa wanasiasa wa Burundi walioko uhamishoni Ubelgiji wamekubaliana kuunganisha nguvu na kuchukua silaha ili kupindua serikali ya Gitega ambayo hawaheshimu raia wao na hawako tayari kwa mazungumzo ya kuijenga nchi.

Aliendelea kusema kuwa watatafuta washirika ndani ya Burundi walio tayari kujitolea kwa ajili ya kulikomboa taifa lao. Alisema wananchi wana haki ya kuipinga serikali isiyofanya kazi zake.

“Serikali inapokiuka haki za binadamu, raia wana haki ya kuchukua silaha na kuiangusha,” alisema na kusisitiza kuwa watafanya kila kinachowezekana kutimiza azma yao.

Wapinzani hawa wapya wanaojiandaa kwa vita wanajiunga na makundi mengine ya silaha kama vile Red-Tabara, FOREBU, na mengine mengi yanayopambana na serikali ya Burundi.

Mnamo Machi mwaka huu, kundi lingine la kisiasa, FRB-Abarundi, lilitangaza kuungana na UPR na UPF kupinga serikali ya Gitega kwa madai ya ukiukaji wa haki za binadamu na kupuuza raia.

Sangiza iyi nkuru

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *